Sunday, February 22, 2009

Kikao cha Jumuiya March 1,2009

Watanzania wa Canton,
Kutakuwa na kikao cha jumuiya March 1,2009 nyumbani kwa Abeid saa kuanzia saa kumi kamili jioni wote mnaombwa kufika bila kukosa.

Agenda:
  • Kusisitizia michango ya mwezi kwa wale ambao wana outstandings balance from last year.Wanachama mnaombwa kuwa mmemaliza michango yenu kabla ya kikao kijacho.Mwenyekiti Martin ataelezea mada hii.

  • Kuongelea suala la party ya usiku wa mwafrika kama itakuwepo ama la Ndg Msangi na kamati yake watalielezea.

  • Mwaka jana wakati wa ufunguzi wa Umoja Makamu Mwenyekiti Bw.Mohammed Sultan aliongelea katika hotuba yake kuwa umoja utakuwa karibu zaidi na wana umoja kujua info nyeti ili ziweze kuhifadhiwa ili inapotokea jambo tuwe tunataarifa nini cha kufanya mfano mwana umoja mwenzetu kufariki nk.mjadala uko wazi kwa kila Mwanachama kuchangia.........

  • Pia tulizungumzia katika kikao cha mwisho jinsi ya kuwasaidia au kusaidiana kila mwana umoja apate health insurance,suala zima la health care,umuhimu wa kufile tax na pia kufuatilia suala la memorial funds info ziwe available kwa umoja.Kama ambavyo tuliweza fanikisha suala la wanasheria kuwa available kwa kila mwanachama tunatafuta njia ya hii mada iwe hivyo.Mada hii Ndg.Ngwilizi ataielezea since ana utaalamu wa kutosha.

  • Mada ya mwisho itakuwa kuangalia masuala ya legal papers za wamachama kuwawezesha kuishi na kufanya kazi kihalali USA.Mada hii itawalenga tu kwa wale ambao wako wazi kushare na umoja kuweza kusaidiwa kimawazo katika vizingiti wanavyopitia kuelekea kushinda kesi zao.Umoja uko proudly kwa baadhi ya wanachama ambao wameleta kesi zao na zimekuwa zinafuatiliwa kwa karibu na chache zimeenda vizuri sana.Katibu ataiwakilisha hii.

Katibu.....



Saturday, February 14, 2009

Viwanja na Nyumba vinauzwa

Wadau,
Kwa wale wanaotembelea blog hii kuna viwanja na nyumba vinauzwa na si mbali bali ukitembelea blog yetu nenda sehemu inasema Blog follower au follower click hapo utaona kila dizaini na maeneo uyatakayo kwa ajili ya finali nyumbani.

HAPPY VALENTINES DAY

Watanzania wa Canton Ohio na duniani kwa ujumla.

Watanzania wa Canton, wanawatakia heri na fanaka katika kusheherekea sikukukuu hii ya wapendanao duniani.Love one, love all!! Tujenge muelekeo mpya mwaka huu wa 2009 kuumba sura mpya ya UPENDO kati yetu.

Mungu atusaidie!!!

Saturday, February 7, 2009

Watanzania Canton Ohio kwa pamoja tutaendelea!!





Watanzania wa Canton wakiwa pamoja nyakati zote za raha na shida.We are family here in Canton...Lets keep our motto!!