




Father Malasi.
Father Malasi amekuwa na umoja wetu wa Watanzania waishio ukanda wa kaskazini kwa zaidi ya miaka 7 hivi na sasa umefikia wakati au hatma ya Father Malasi kurudi jimboni nyumbani Tanzania kumtumikia Mungu.Father huyu amekuwa nasi hapa kishule na ameweza kumaliza elimu yake ya juu ya Ph.D katika ukanda wa kemia.Umoja wa Watanzania waishio Canton Ohio wanayo furaha kubwa na kumpongeza kwa mafanikio yake na pia kuonyesha upendo na umuhimu wake wa kitume kati ya wana umoja kwa muda wote huu tulio ishi nae hapa.Pia tulipata nafasi ya kukutana na mkuu wa jimbo la Moshi mjini Baba Askofu Isaac Massawe ambae aliongea na watanzania na pia kuonyesha umuhimu wa Father Malasi katika jimbo la Moshi pindi atakapowasili Tanzania.Tungependa Father Malasi aendelee kuwa nasi ila muda nao umetutupa sharti arejee nyumbani kwa majukumu mengine ya kitawa.Mungu ubariki umoja wetu, Mungu mbariki Father Malasi, Mungu ibariki Tanzania..