Monday, May 10, 2010

Happy Mother's day

Happy Mother's day to all our Tanzanian sisters here in Canton and around the globe.

Greetings from T.A.C

Wednesday, December 16, 2009

NEW YEAR EVE PARTY

Tired of bringing in the new year in the same way every year?
Make this year a year to remember! The Tanzania Associan of Canton presents,
a New Year bash at Lollies Banquet hall of Belden Village.
$5.00 cover charge at the door. Food, drinks, and fun!
Music by DJ Kvelli of Columbus. Rap, Hip-Hop, and much more!
Call 330-418-6401 or 330-575-7148 for V.I.P and info.
Lolli's Restaurant and Banquet Center4801 Dressler Road NW.Canton, Ohio 44718Call: 330.492.6846Toll Free: 1.877.GOLOLLI(1.877.465.6554)Fax: 330.492.0836lollisrestaurant@aol.com

Tuesday, November 24, 2009

Mnuso wa Nguvu Canton Ohio

Watanzania wa Canton wanayo furaha kuwakaribisha watanzania wote waishio Canton Ohio na vitongoji vyake kwenye kusheherekea pamoja nasi siku kuu ya Eid El Hadji siku ya Ijumaa saa kumi na nusu jioni 4:30pm kwenye Ukumbi wa kisasa wa Saifert Flower Mill 7300 Wales Rd North Canton. Muziki utangurumishwa na Dj Mo.... vyakula asilia vya kumwaga na vinywaji mtindo mmoja.Upatapo taarifa hii mfahamishe na mwingine.

Karibuni sana

Kamati ya Maandalizi

Saturday, October 10, 2009

Sheikh Mohammed kapata Jiko












Sept 26,2009 siku ndg yetu Mohamed Khalid Sultan alipopata mwezi wake wa maisha.....ilikuwa ni nderemo na vifijo.Wote waliohusika na shughuli hii shukrani za dhati ziwaendee wote....Inshallah.




Saturday, July 11, 2009

Bon Voyage Father Malasi

















Father Malasi.
Father Malasi amekuwa na umoja wetu wa Watanzania waishio ukanda wa kaskazini kwa zaidi ya miaka 7 hivi na sasa umefikia wakati au hatma ya Father Malasi kurudi jimboni nyumbani Tanzania kumtumikia Mungu.Father huyu amekuwa nasi hapa kishule na ameweza kumaliza elimu yake ya juu ya Ph.D katika ukanda wa kemia.Umoja wa Watanzania waishio Canton Ohio wanayo furaha kubwa na kumpongeza kwa mafanikio yake na pia kuonyesha upendo na umuhimu wake wa kitume kati ya wana umoja kwa muda wote huu tulio ishi nae hapa.Pia tulipata nafasi ya kukutana na mkuu wa jimbo la Moshi mjini Baba Askofu Isaac Massawe ambae aliongea na watanzania na pia kuonyesha umuhimu wa Father Malasi katika jimbo la Moshi pindi atakapowasili Tanzania.Tungependa Father Malasi aendelee kuwa nasi ila muda nao umetutupa sharti arejee nyumbani kwa majukumu mengine ya kitawa.Mungu ubariki umoja wetu, Mungu mbariki Father Malasi, Mungu ibariki Tanzania..





Friday, June 26, 2009

Mtanzania ndani ya NBA Hasheem Thabeet




Hasheem Thabeet aiweka Tanzania kwenye ramani ya mpira wa kikapu....Watanzania wa Canton Ohio tumefurahishwa sana na tukio hili la kihistoria....Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Hasheem...!!!








Tuesday, May 26, 2009

RAIS KIKWETE WA TANZANIA AWA RAIS WA KWANZA WA AFRICA KUKUTANA NA OBAMA


Rais Kikwete awa rais wa kwanza wa Africa kukutana na Rais Barack Obama wa Marekani.