Wednesday, December 31, 2008

Kimaso maso mwanetu huyo!!

Keki rasmi ya umoja ikishuhudiwa na wana umoja

Happy New Year 2009

Heri ya mwaka mpya kwa wanajumuiya Tanzania ndani ya nje ya Canton Ohio.TAC inatoa salamu za pekee kwa kila mwanachama wake na watanzania wote kwa ujumla nje na ndani y Canton ohio.
Tunamuomba mola atuwezeshe kuvuka mwaka 2008 salama na kuuona mwak 2009 kwa nguvu na ari na kasi mpya.Umoja wa watanzania TAC unawatakia wote wasomao blog hii Heri ya mwaka mpya na mwaka huu wa 2009 uwe ni mwaka wa mafanikio tele.Fuata sheria za nchi,fuata sheria za barabarani, zingatia mambo muhimu katika maisha yako,panga kuwa mmojawapo wa waletao maendeleo kwa umoja na kwa wana umoja.Panga kuwa mstari wa mbele kuhudhuria vikao vya umoja na kutoa michango yako ya mawazo,kifedha na kihali nje na ndani ya umoja.Mpende mwana umoja mwenzako na asiye mwana umoja na kumtakia mema na asiye mwanachama mfahamishe kuhusu umoja wetu.
Asanteni sana
Viongozi

Wana umoja wakila happy za ufunguzi wa Umoja

Libeneke likiendelezwa!!

Matukio katika Picha za ufunguzi wa umoja


Makamu Mwenyekiti akikata keki kuwalisha watoto ambao wawakilishi wa baadae wa umoja wetu

Taarifa ya Kikao cha December 6,2008

Ndg watanzania wa Canton Ohio.
Ifuatayo ni taarifa ya kikao cha December 6,2008.
Waliohudhuria,
Edgar Lema
Joe Ngwilizi "Mzee wa Njegele"
Mohammed Sultan
Juma Msangi
Frank Chungu
Judy Weir
Abeid Rashid
Shabani Kilongola
Giliard Msangi
Jimmy Msemo

Waliotoa Udhuru
Edna Ngowi
Martin Yohana
Calistus Rwejuna
Dada Hadija
Abuu Alkanaan
Kombo "Dawa"
Seleman Farouq

Kikao kilichelewa kuanza kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na taarifa ya kikao kuwa kingefanyika tarehe 6 haikuwafikia wengi kwa wakati muafaka.
Hivyo iliamuliwa kuanzia Dec 6,2008 vikao vyote vya umoja vitakuwa vinafanyika Jumapili ili kuweza kuwa uhuru wa wengi kuhudhuria vikao.

Kikao kilifunguliwa na Makamu Mwenyekiti Ndg Mohammed Sultan ambaye anakaimu nafasi ya Mwenyekiti mpaka hapo uchaguzi wa nafasi zilizoachwa wazi zitakapojazwa.

Makamu Mwenyekiti alianza kwa kuwashukuru waliofika kwenye kikao licha ya hali mbaya ya hewa kuwepo siku hiyo.

Alitoa nafasi ya watu kuweza kuchangia hoja ya kuangalia suala la uchaguzi kwa kuwapa nafasi wajumbe waweze kuchangia maoni yao ni vipi tuangalie jinsi ya kuchagua mwenyekiti wetu wa umoja kwa kutokuangalia sura wala ukaribu wetu au mengineyo.Wajumbe walichangia hoja hii kwa upana zaidi kwa kukubaliana kwa kauli moja kuwa kila mmoja afanye jitihada za kuangalia sifa za mwenyekiti kwa kuangalia umuhimu wake katika chama na watu binafsi,kuangalia misimamo yake,kuangalia tabia yake,kuangalia mienendo yake,na ushujaa wake katika kuongoza na maamuzi na kuwa mtu wa watu pale anapohitajika kufanya ndani na nje ya chama.

Pia Makamu Mwenyekiti alisisitiza kuwa umoja utaendelea tu hata kama yeye Mohamed atatoka haimaanishi basi na umoja ufe pia alidokezea kwa kusema tunapopitia mitihani ndio inatuimarisha zaidi hata miaka ya baadae hatuwezi kurudia matatizo tuliyoyapitia.

Wajumbe walipendekeza kuwa kipengele hiki kiongezwe katika katiba Kiongozi yeyote anapoachia ngazi basi aliyechini yake ni budi achukue madaraka mpaka hapo uchaguzi utakapoitishwa tena.

Pia kulikuwa na agenda ya kuhusu wana jumuiya kuangalia email zao na kuzijibu pale inapobidi.Kumekuwa na mtindo wa watu kuchambua email au text kwa uchambuzi wao either kwa nia nzuri au mbaya kikao kiliamua kuwa wajumbe wajaribu kujibu hizo email kwa mhusika kumfahamisha ili kama kuna marekebisho yafanyike mara moja badala ya wajumbe kuzunguka kwenye vikao ambavyo si halali vya jumuiya kuongelea mambo yahusuyo jumuiya au kiongozi au mwanachama.Tuliamua kuunda umoja wa uwazi na ukweli ndivyo ambavyo tutashinda mitihani yote inayoikabili jumuiya.

Umoja na wanajumiya walipokea taarifa ya account ya bank ambayo ilipata upinzani mkali toka kwa wajumbe wakitaka maelezo ya kina toka kwa viongozi jinsi account ilivyofunguliwa.Viongozi walitoa maelezo ya kutosha kwa wajumbe process nzima ilivyokwenda.Sasahivi tuna account ya umoja pale Firstmerit Bank iko chini ya jina la Tanzanian Association of Canton Ohio (TAC).Kwa mujibu wa katiba yetu tunatakiwa tuwe na signatory watatu kufungua account ya umoja na bank walitaka watu watatu,Tax ID form,na Registration ya umoja.Haya yote yaliwezwa kufikiwa na account kufunguliwa rasmi mwezi wa Novemba 2008.Kutokana na timing ya kuifungua ilibidi Mwenyekiti wa kamati ya Fedha kufanya kila awezalo ifunguliwe mara moja yeye anaweza kufanya mabadiliko yeyote kama yatahitajika hivyo.

Website ya umoja iko bado kwenye matengenezo tutapokea ripoti yake karibuni.Maelezo yote yanayotakiwa kwenda kwa website yameshawekwa tayari na viongozi wote walitumiwa na wakayaapprove.

Michango na Mahudhurio: Wajumbe walisisitizia sana suala la wajumbe wengi ambao hawafiki kwenye vikao kwa muda mrefu.Iliamualiwa wajumbe hao wengi ambao hawajafika kwenye vikao muda mrefu ufanyike mpango wa kuwafikia na kujua matatizo yao ni nini ili umoja uwe na taarifa ya kinachoendelea.Imeonekana kuwavunja moyo wengi ambao wamekuwa waaminifu kuitikia mwito wa vikao vinavyoitishwa vya mara kwa mara vya umoja na wengi wao hawahudhurii inaonekana kuwavunja moyo wana umoja na viongozi pia.Tulianzisha jinsi ya kufikisha ujumbe kwa njia ya email na text msg na simu na mara nyingi ujumbe ule unaishia na kusema "ukipata ujumbe huu mfahamishe na mwingine" huu ndio motto wetu na wengi wamekuwa wakifikisha ujumbe tunashukuru sana kwa kuweza kutusaidia kwa hilo.

Michango iliamuliwa kwa wale ambao hawajamaliza michango yao ya umoja ya kila mwezi wafanye hivyo kabla ya mwisho wa mwaka na wale ambao hawajamalizia hela zao za kiingilio wafanye hivyo pia ili tumalize mwaka kwa nguvu tuingiapo mwaka 2009 tuuanze kwa kishindo kikubwa.

Wajumbe walikubaliana kwa kauli moja kuivunja kamati ya usuluhishi na matatizo na iliamuliwa matatizo yote yafikishwe kwa viongozi kuanzia sasa.Wajumbe waliongezea kwa kusema mpaka sasa matatizo yote yamekuwa yakitatuliwa na viongozi na yaendelee tu.Suala hili lilipitishwa kwa kauli moja since katiba inasema nusu ya wajumbe wakipiga kura ya kukataa au kukubali inakubalika kikatiba.Jumuiya ina wajumbe active 16 waliohudhuria walikuwa 9 tuko zaidi ya nusu ya wanajumuiya so hoja hii ilipitishwa kikatiba.

Makamu Mwenyekiti aliwapongeza sana wajumbe kwa kuitikia miito ya umoja pale kunapokuwa na wagonjwa au vifo au furaha kwa kweli wanajumuiya ya Canton wamekuwa mstari wa mbele sana.Mifano mizuri Andrew alipofiwa,Bahati alipofiwa,Selemani alipofiwa,Greg anayeuguliwa,Calistus harusi yake,Edgar alipofiwa huko Columbus,Graduation Tenessee,Edna Ngowi na Ngwilizi babyshowers nk.Tunaomba tuendeleze moyo huu huu katika hali zote tunazokumbana nazo.

Pia wajumbe walikubaliana kuwa mwenyekiti wa zamani afikishiwe ile barua aliyoandika ya kujiuzulu aweze kuisaini kwa ajili ya kumbukumbu za UMOJA kuweza kuondokana na usumbufu unaoweza kutokea.

Pia tuliangalia mafanikio mengi tuliyoyafikia kama wanajumuiya natunampongeza Mwenyekiti wetu wa zamani Kilian Kamota kwa kuweza kutuongoza vyema kufikia tuliyofikia na kwa kauli moja wana jumuiya tulimtakia mafanikio mema.

Pia tuliangalia suala la kufunga mwaka na ufunguzi rasmi wa jumuiya ambapo kutakuwa na party Dec 20.2008 nyumbani kwa Bwana Giliard Msangi kuanzia saa moja jioni mpaka liamba.Kwa wajumbe ambao hawajatoa michango yao wanaombwa kufanya hivyo ASAP muda tuliobaki nao ni mdogo sana.Tarehe 19 december 2008 tuliombwa kufika kwa Giliard jioni kwa ajili ya usafi nadhani Bwana Joe na Martin watatuongoza katika suala hili wakishirikiana na Giliard jinsi ya kuandaa mahali na mpango wa kupata viti kuweka mandhari tayari kwa kupasua jipu.Mchango ni dola 25 tu kwa mtu tukiweza kutoa michango yetu mapema inarahisisha upangaji wa sherehe kujua nini kiwepo na nini kisiwepo.Wasiliana na waandalizi wa sherehe hii ndg Joe na Martin.

Tulipata muda wa kuangalia mambo tutakayoanza nayo mwakani.Ndg.Ngwilizi ana mpango wa kutuletea kampuni ya Primeamerica waje waongee nasi kuhusu masuala ya Life insurance,budgeting,health insurance nk tutawafahamisha.Pia wajumbe ambao hawana Prepaid legal waliombwa wafanye hivyo wajiandikishe tuna mwakilishi hapa Bwana Martin Yohana fika muone upate fomu na maelezo yote.

Pia tuliongelea suala la umoja kujua mambo muhimu ya wana umoja just incase mwenzetu anatutangulia umoja una taarifa gani zozote za kuhusu mhusika arudishwe nyumbani au azikiwe hapa hapa tutayaongelea kikao cha kwanza cha mwakani.
Tulizungumzia mambo ya memorial funds nk tunayapataje mwakani tukija kukutana tutakuwa na taarifa za kutosha tutakapokutana jaribu kuandaa info na idea za kutosha.

Katibu alimalizia kwa kusema umoja huu tunaujenga si kwa faida yetu au kwa ajili yetu tu bali tunajenga legacy ya watoto wetu mfano mzuri Rais mteule Obama ametupa changamoto hata watoto wetu tuliozaa ugenini wanaweza kuwa watu fulani pale tu tutakapoweka misingi mizuri ya umoja au kuwawekea misingi mizuri ya kuuendeleza umoja.Inawezekana kabisa Mwenyekiti wakaja kuwa watoto wetu na wakatumia opportunity hii kuelekea matawi ya juu kama ndg yetu na rais wetu Obama.Aliomba tuliangalie suala la umoja kwa upana zaidi na si pua na mdomo tu tufunguke macho na tuone mbali zaidi tusiangalie jana wala kesho

Thursday, December 25, 2008

Ufunguzi wa Umoja wa Watanzania waishio Canton,Ohio

Umoja wa Watanzania Canton Ohio Tanzanian Association of Canton, Ohio TAC.
Ni umoja ambao uliasisiwa au ulianzishwa na waasisi wa Umoja huu na kuweza kufikia hatima ya kufunguliwa rasmi December 20,2008 tukio la kihistoria hapa Canton Ohio.
Tukio hili la kipekee lilianza kwa kufunguliwa na Mwenyekiti wa muda Bwana Mohammed Sultan kwa kutoa utambulishi wa wanachama wote na pia kutoa historia fupi ya umoja huu tokea kuanzishwa kwake.Pia Mwenyekiti alitoa mafanikio ya mpaka sasa yaliyofikiwa na umoja na jitihada zake zote ambazo zimepelekea kufikia kilele cha kuanzisha umoja huu na matatizo ambayo wameweza kuyapitia kama wana umoja na kuyashughulikia kufikia masuluhisho yake kwa fanaka ya hali ya juu.
Mwenyekiti wa muda alikata utepe kuashiria kuanzishwa kwake rasmi tukio ambalo lilishuhudiwa na wanachama kwa furaha kubwa huku wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania.Pia ilikuwepo keki kubwa ambayo ilikatwa na kulishwa watoto kwa niaba ya wana umoja wote kuashiria tunajenga legacy kwa ajili ya watoto wetu watanzania tuliowapata ugenini kuweza kuja kuendeleza umoja wetu huu.Kama anavyosema Rais mpya wa America "success comes from bottom up" ndio nia yetu tunayolenga ianze kwa watoto wetu kuweza kufikia kufanya ordinary things to extraordinary.
Wanachama walipata fursa pia ya kuongea mengi yanayohusu umoja na kuona picha halisi ya future ya umoja kuanzia 2009 malengo haswa ya umoja kama walivyoyadiscuss katika kikao kilichopita cha Dec wanachama walilenga kufanya mengi makubwa kuliko waliyoyafanya kwa mwaka 2008.
Wana umoja kwa kauli moja walikubaliana mwaka 2009 uwe ni mwaka wa mafanikio na moto zaidi katika kufanikisha malengo ya chama nje na ndani ya chama.Kujenga amani zaidi na kulenga zaidi upendo ndani ya wanachama.Kuongeza idadi ya wanachama iwe kubwa zaidi haswa wadada wetu.
Pia wanachama waliombwa kuhudhuhuria vikao vinavyoitishwa na chama kwa wingi ili kujenga misimamo ya chama kwa pamoja.