Monday, January 26, 2009

Taarifa ya Uchaguzi T.A.C

Watanzania,
Ifuatayo ni taarifa ya kikao kilichofunguliwa saa kumi kamili na kilitanguliwa na kikao cha viongozi kilichoanza saa tisa mchana.
Makamu mwenyekiti alidokezea mambo machache kuhusu umoja
Michango ya umoja ya kila mwezi na ya kujiunga
Kusoma email na text messages
Nidhamu ndani ya mikutano kuanzia leo kutakuwa hamna vinywaji wakati wa vikao vinywaji vitanyweka baada ya kikao kumalizika.
Simu zetu tuweke kwenye vibrate ili kuondoa usumbufu wakati wa mikutano
Pia watu waonane na Joe kuweza kufile Tax
Ufafanuzi wa Party ya usiku wa Mwafrika
Pia chama hakitatoa mikopo kwa mwanachama kwa sasa mpaka hapo itakapotangazwa.

Katibu alisisitiza amani na upendo na tuondoe tabia ya chuki mbaya au maugomvi mabaya tuliyonayo baina yetu.Tujenge hulka ya kujaliana badala ya kutakiana mema.Mwenzako anapopata matatizo basi isiwe ndio nderemo na vifijo bali iwe ni jinsi gani utamsaidia?

Uchaguzi
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi alianza rasmi kwa kuwakumbushia wanachama kuchagua wagombea kwa nia ya kuchagua kiongozi anayefaa na si kwa jina au sura.
Uchaguzi ulianza wa nafasi ya mwenyekiti iliyoachwa wazi na ndg Kilian Kamota.Nafasi hiyo ilikuwa inagombewa na Bwana Martin Yohana na Giliard Msangi na Bwana Martin alishinda nafasi hiyo.
Mwenyekiti mpya wa umoja ni Martin Yohana.

Nafasi ya katibu wa Fedha
Wagombea walikuwa Calistus Rwejuna na Edna Ngowi na nafasi hiyo ilichukuliwa na Bwana Calistus Rwejuna

Nafasi ya Mawasiliano Mwenyekiti
Nafasi hiyo ili ilikuwa inagombewa na Juma Msangi na Giliard Msangi ambapo Bw.Giliard alijitoa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa tayari anayo madaraka mengine ndani ya chama na Bw.Juma Msangi alipita kwa kura zote za ndio

Nafasi ya Mawasiliano Katibu
Nafasi hiyo ilikuwa inagombewa na Abeid Rashid na Seleman Vuai na Bw.Abeid alishinda nafasi hiyo.

Katibu alimpa Mwenyekiti mpya taarifa ya umoja tokea kilipoanzishwa mpaka kilipofikia na malengo yaliyopangwa awali yalifikiwaje na tunapoelekea kama wanaumoja tunaelekea wapi.

Mwenyekiti mpya Bw.Martin Yohana alipata nafasi ya kuongea na wanajumuiya kwa kuhakikisha kuwa Umoja utadumishwa kwa amani na kwa nguvu zake ataendeleza kazi zote ambazo umoja ulishazianza hapo awali.Na alisisitiza kuwafikia na wenzetu wa visiwani kwa kuwawezesha kuja katika umoja pia.
Aliahidi kuendeleza mshikamano ndani ya umoja na nje ya umoja na kuendeleza upendo baina yetu.

Pia aliteua washauri wake kumshauri mambo katika uongozi wake nae ni Dada Edna Ngowi na Bw.Joseph Mushi.Na wajumbe waliafiki msimamo wake baada ya kuelezea kwanini amewateua hao wandugu.

Pia alisisitiza matatizo binafsi ya wanachama yasiletwe ndani ya jumuiya kuepuka malumbano na mlolongo wa matatizo.Aliahidi kuonana na wahusika kufikia muafaka wa kila tatizo kuanzia muda aliokuwa akiongea.Pongezi kwa wote waliogombea na pongezi kwa wote walioshinda.Umoja na Amani viendelee kudumu kati yetu.

Katibu.

No comments: