UCHAGUZI WA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI JANUARY 25 ,2009 jioni saa kumi.
Heri ya mwaka mpya!!
1.Watanzania wa Canton.Jumapili ya tarehe 25 January tutakuwa na mkutano wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa Umoja wetu wa Watanzania Canton.Mahali nyumbani kwa Bw.Abeid Rashid.
Ujumbe huu mnaombwa kumfikishia kila mwanachama wa umoja huu na mwanachama yeyote anaombwa asikose kuhudhuria kikao hicho mtumie email tena au mtextie au mpe ujumbe kwa mdomo kila mwanachama ili tupate mtu ambaye kila mtu anaridhika nae na wote tunampenda na awe mtu wa watu na asiwe mtu wa majungu na asiwe muanzisha matatizo kati ya jamii awe mtu imara asiye na papara za maamuzi yake hizi ni mojawapo tu ya sifa za Mwenyekiti wetu mpya najua kila mtu anasifa anazohitaji mwenyekiti awe nazo.Kitakuwa ni kikao cha uchaguzi tu wa viongozi waliotajwa na kamati ya uchaguzi.Uchaguzi utakuwa saa kumi jioni nyumbani kwa Abeid.
2.Kikao hiki kitaendeshwa na Mwenyekiti wa muda na kitasimamiwa na Kamati ya uchaguzi na wao watatupa kamati zinazohitaji kupata viongozi wapya.Tunaomba majina yawezwe kupitiwa mapema kabla ya kikao.
3.Kutakuwa na updates za kikao rasmi kijacho cha kwanza cha jumuiya kuendeleza libeneke la umoja wetu.
4.Umoja ni nguvu TAC idumu!!
Katibu.
Friday, January 2, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment