Thursday, January 8, 2009

Wasaha toka Bw.Martin Yohana

WARAKA KWA WATANZANIA WAISHIO CANTON
NDUGU WATANZANIA WENZANGU WOTE ,NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUWAPONGEZA KWA MSHIKAMANO TUMEO UONYESHA KATI YETU SISI KAMA JAMII MOJA YA WATANZANIA.NI KWA MUDA MFUPI SANA TUMEWEZA KUFAULU KWENYE MAMBO MENGI YA MSINGI YANAYO TUZUNGUKA, KITU AMBACHO KINAONYESHA BISHARA NZURI YA MUUNDO NA MUELEKEO MZIMA WA JUMUIYA HII NA WATU WAKE AMBAO NI SISI WENYEWE.
JAPO KUWA SISI WATANZANIA TUISHIO HAPA CANTON NI WACHACHE UKILINGANISHA NA STATES AU VITONGOJI VINGINE,NI DHAHIRI KUWA UCHACHE WETU NA UCHANGA WA JUMUIYA YETU UMEONYESHA KUWA NA NGUVU ZAIDI KULIKO JUMUIYA NYINGINE NYINGI NA ZENYE WATU WENGI HAPA MAREKANI.NGUVU HII INATOKANA NA UPENDO WA HALI YA JUU KATI YETU.HATUA MOJA BAADA YA NYINGINE ,TUNASONGA MBELE.,IWE NI SHEREHE,MSIBA,AU DHARURA YOYOTE ,SISI WANA CANTON NA UCHACHE WETU HUU,HUWA NI WAKWANZA KUITIKIA MIITO HIYO POPOTE PALE PANAPOTUZUNGUKA KWA UKARIBU.HIVYO NAOMBA TUJIVUNIE KWA UPENDO ,UNDUGU NA MSHIKAMANO TULIOJIJENGEA.
NAPENDA PIA KUTAMBUA MCHANGO WA MWANAJUMUIYA MWENZETU,MDAU HUYU AMEKUWA MSTARI WA MBELE KWENYE MAFANIKIO YA WENGI.BILA MASHARTI ,MWENZETU HUYU NI SHUPAVU,BUSARA YA HALI YA JUU NA HUTUMIKIA JAMBO LA MTU YOYOTE KWA MOYO MWEUPE NA HU HAKIKISHA AMETIMIZA WAJIBU WAKE KWA KAZI ANAYOKUWA AMEAGIZWA.HUYU SI MWINGINE ILA NI NDUGU YETU FRANK CHUNGU.
TUNABAHATI ILIOJE KUWA NA JASIRI AU SIMBA WA NYIKA,SHAULING WA BUSARA NA HEKIMA.MDAU HUYU AMEENDELEA KUTUFAA SISI SOTE KWA MASHAURI MBALIMBALI NA JINSI TUNAVYOTAKIWA KUISHI KWA KUFAHAMIANA, KUHESHIMIANA NA KUVUMILIANA KAMA BINAADAMU.MDAU HUYU NI HADHINA KWENYE JAMII YETU NA TUTAMLINDA KAMA MZEE WETU,HUYU SI MWINGINE BALI NI USTAADH SHEIK MOHAMED SULTAN.
MABADILIKO YA SERIKALI YA TANZANIA YANA DREAM YA KUCHUKUA SURA MPYA YA UONGOZI BAADA YA SISI WANA CANTON KUMPIKA IPASAVYO RAISI MTARAJIWA WA SERIKALI YETU YA TANZANIA MIAKA MICHACHE IJAYO, HUYU NI MDAU TUNAE TAKIWA TUJIVUNIE SANA KUWA NAE KARIBU KWA BUSARA ZAKE, UKUBWA WA MITAZAMO YAKE KWENYE DUNIA YA SASA,UFANISI WA KAZI ZAKE BINAFSI NA ZA JUMUIYA YETU.HUYU NI SILAHA YETU YA SIRI NA SI MWINGINE BALI NI MUHESHIMIWA JOSEPH M.NGWILIZI.
GILLIARD MSANGI NA JOSEPH(DIDAS)MUSHI,HAWA MIMI NI VIJANA WANGU,NA WATU WANGU WA KARIBU.HAWA VIJANA NI SAFI,NI DAMU CHANGAMOTO KWENYE UMOJA WETU.NI VIJANA WENYE PEO ZINAZOKWENDA NA WAKATI.MIMI NINAIMANI KUBWA KUWA TUTAPATA MAWAZO SAFI NA MUELEKEO MWEMA WA CHAMA KWANI MUSWAADA WOWOTE MZURI HUPITA BAADA YA KUWA UMEFANYIWA KAZI NA WAJUMBE WENGI WENYE MAWAZO TOFAUTI ,NA HILI TUTALIPATA TOKA KWA WADAU HAWA.
JAPO KUWA NAO NI WAKUHESABU, TUNAJIVUNIA PIA KUWA NA DADA ZETU WA KITANZANIA KWENYE UMOJA WETU.HAWA PAMOJA NA MAMBO MENGINE, WAMEKUA NI CHANGA MOTO KWENYE JAMII HII.MICHANGO NA UONGOZI WAO KWENYE JUMUIYA IMEKUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA JAPO KUWA SIKU ZOTE KUNA NAFASI YA KUFANYA ZAIDI KWA MANUFAA YA WOTE KAMA JUMUIYA.TUNAWAOMBA WAENDELEZE USHIRIKA WAO NA WANATAKIWA KUFAHAMU KUWA TUNAWAPENDA SANA KAMA DADA ZETU NA HESHIMA YAO KAMA WANAWAKE INABAKI PALEPALE.
NIKIGUSIA UCHAGUZI UJAO,NINGEPENDELEA SANA KUONA ANACHAGULIWA KIONGOZI MWENYE SIFA ZENYE MANUFAA KWA JAMII NZIMA.KATIBU WA JUMUIYA NGUDU CHUNGU AMELIONGELEA SUALA HILI TAYARI,ILA KWA NYONGEZA NAPENDA KUWAFAHAMISHA WANAJUMUIYA WOTE WA HAPA CANTON KUWA SISI WOTE NI VIONGOZI WAZURI NA YEYOTE ATAKAE CHAGULIWA TUTAMUHESHIMU KAMA KIONGOZI WETU NA TUTATOA USHIRIKA KWAKE ILI KUHAKIKISHA MADARAKA YAKE HAYO YANAWATUMIKIA WANAJUMUIYA WOTE KWA KUFUATA MISINGI YA KATIBA YA JUMUIYA HII.AWE NI KIONGOZI ATAKEYE SIKILIZA KILIO CHA WATU NA AWE MUWAZI KWA MASWALA YANAYOTAKIWA KUWEKWA WAZI.
NDUGU ZANGU TUKUMBUKE KUWA JUMUIYA IWE NI KAMA MTOTO AMBAE ANAKUZWA KWA MISINGI THABITI ILI TUWEZE KUPATA MATUNDA BORA TOKA KWA MTOTO WETU HUYU.TUKIMLEA VIBAYA BASI TUSITEGEMEE CHOCHOTE,.NINAMAANA GANI HAPA?..MAANA YANGU NI KWAMBA KILA MWANAJUMUIYA ANAJUKUMU LA KUIFANYIA JUMUIYA JAMBO JEMA,NI KWAMBA UJIULIZE UTAIFANYIA NINI JUMUIYA? NA SIO JUMUIYA IKUFANYIE NINI?...JAMBO KAMA MICHANGO YA JUMUIYA NI LAZIMA WEWE KAMA MWANAJUMUIYA UTOE ADA ZOTEZAJUMUIYABILAKUFUATWA., MAHUDHURIO YA VIKAO VYA JUMUIYA NI WAJIBU WA KILA MWANAJUMUIYA KUTIMIZA BILA KUSUKUMWA.KWA KUFANYA HIVI TUTAWAPUNGUZIA KAZI VIONGOZI WATEULE, KWANI VITU VINGINE KAMA HIVI, HAVITUHITAJI KUWA WANA SAYANSI KUVIGUNDUA,BALI NI AKILI YA KUZALIWA AMBAYO NAAMINI SISI SOTE TUNAYO AKILI HIYO NA ILIYO TIMIA, HIVYO HATUNA ZINGIZIO LOLOTE.
IWEKWE WAZI KUWA AMBAE HANA NIA YA KUJIUNGA AU KUENDELEA NA UANACHAMA WA JUMUIYA YETU ATAMBUE KUWA YUKO PEKE YAKE(‘’YOU ARE IN YOUR OWN’’....BY Pres. Obama)NI LAZIMA TUWAULIZE WATU HAWA AMBAO WAMEJITENGA ILI KUJUA MITAZAMO YAO KWA MWAKA HUU MPYA KUHUSU JUMUIYA NI VIPI?WATU HAWA WANAFAHAMIKA NA HILI PIA LIWE JUKUMU LA KIONGOZI MPYA KUWA NA KAULI KWA WATU HAWA.
VILEVILE MOJA YA JUKUMU LA UONGOZI MPYA IWE NI KUHAKIKISHA KUWA WATANZANIA WENZETU KUTOKA VISIWANI WANAJUMUIKA KWENYE UMOJA HUU. HII ITACHANGIA KUENDELEZA MSHIKAMANO NA UNDUNGU TULIONAO BAINA YETU.MAONI AU SABABU ZILIZOSIKIKA AWALI TOKA KWA WATANZANIA HAWA WA VISIWANI KUHUSU NI KWANINI HAWAJAJIUNGA MPAKA SASA ,YAFANYIWE KAZI. NA PANDE ZOTE MBILI ZIFIKIE MUAFAKA UTAKAO KIDHI MAHITAJI YA PANDE ZOTE.HILI NI JAMBO MUHIMU SANA NA TULIZINGATIE KWA AJILI YA KUIMARIKA KWA UMOJA WETU.
NAAMINI KIKAO KITAENDA SALAMA NA KITAKUWA CHA MAFANIKIO.PONGEZI KUBWA KWA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI BWANA ZITTO a.k.a BENA KITU,KWA KUTUPA MUDA WA KUJIPANGA NA HATIMAYE KUFIKIA SIKU YA KUMCHAGUA KIONGOZI MWINGINE. SHUKURANI ZIWAENDEE WAJUMBE WOTE AMBAO SIKUWATAJA KWENYE WARAKA HUU,HII HAINA UBAGUZI WA AINA YOYOTE,TOKA MOYONI MWANGU NI KUWA NINAWAPENDA WOTE ,NA WOTE SISI NI WANA WA MUNGU NA MICHANGO YENU KWENYE DUNIA HII TUNAIHITAJI SANA KUSHINDA KITU CHOCHOTE.ASANTENI SANA.
MARTIN.

1 comment:

Anonymous said...

Sasa ndugu zetu wa Canton mbona mnaandika issues zisizo na mwelekeo? Watch your words... Mara Rais mtarajiwa mara sijui nini.. Acheni kuota ndoto za mchana.