Saturday, March 14, 2009

Mipangilio ya Umoja 2009

Muendelezo wa majadiliano ya nyongeza katika kikao kilichopita........

Wajumbe waliongelea suala la umoja kujishirikisha katika nyanja mbalimbali katika community ya Canton.Mojawapo ya mambo ambayo tuliweza yaongelea ambayo kama wana umoja tukania mamoja kwa nia moja na yenye malengo mema yanaweza kuwa ndio ufunguo wa mengi mbeleni kwa wana umoja na umoja kwa ujumla.
(1)Tuliongelea suala la umoja uandae muswada ama barua ya kupeleka kama mahospitali mfano Aultman,Doctors hospital na Mercy,au Godwill,Salvation Army,City of Canton,Walmart,shule,Mayor's office n.k kwa wana umoja kupitia umoja kuchukua muda wao na kwenda kujitolea kufanya kazi au lolote wanalopenda sisi tuvolunteer ili kujenga jina la uaminifu katika umoja wetu na pia kujenga uhusiano wetu na hizo organization nyingine ili pindi inapofika wakati umoja unahitaji msaada wa wana umoja kupata kazi au kama maafa yamefika Tanzania mfano magonjwa,mafuriko,janga la njaa,hospital zinahitaji vitanda Tanzania,au shule zinahitaji vitabu au computer au lolote inakuwa kuwa urahisi maanda tayari umoja ushajenga daraja na hizo organization kwa sisi tu kujitolea muda wetu kufanya kile kidogo wanachotaka tukifanye.Hili lilipokelewa na wana umoja kwa vizuri sana sasa suala lilikuwa how to execute the idea....Napenda kuwakilisha tena kwa wana umoja waliohudhuria na wasiohudhuria kikao kilichopita kuendeleza mchakato huu.........wadau mpo tunahitaji maoni yenu..

No comments: