Friday, March 13, 2009

Taarifa ya kikao cha 3.1.2009

Watanzania wa Canton,

Kwa niaba ya Mwenyekiti na viongozi wenzangu napenda kuwakilisha taarifa ya kikao chetu cha kwanza kwa mwaka 2009 kilichofanyika mwezi wa 3.1.2009 nyumbani kwa Abeid Rashid.

Waliohudhuria:
Martin Yohana
Seleman Vuai
Edgar Lema
Mohamed Sultan-awamu ya kwanza ya kikao
Evarist Muhaya
Juma Msangi
Frank Chungu
Abeid Rashid
Edna N.Robinson
Oliva Kavishe-toka Columbus
Isaac Lyatuu-toka Columbus
Cecilia Ngowi
Said Said
Didas Mushi

Wasiohudhuria:
Giliard Msangi-udhuru
Lester Zito
Jimmy Msemo
Dawa Kada-Safarini Tanzania
Abuu
Judy Weir-mgonjwa
Rose Richard-alisindikiza mgonjwa Judy hospital

Agenda ya kwanza:
Ilikuwa ni kusisitiza michango agenda hii Mwenyekiti wetu Bw.Martin Yohana alikubaliana na kamati ya Fedha naye awepo kwenye mchakato wa kufuatilia kwa ukaribu wale wote ambao hawajamaliza michango yao ya awali ya 2008 na ya viingilio.Tunapenda kuweka wazi kuwa zoezi hili lilikwenda vizuri sana na michango mingi iliweza kuwakilishwa na wajumbe kabla ya mkutano na panapo mkutano wa jumuiya wajumbe waliweza itikia mwito huo.Mwenyekiti pia alisisitiza watu kutoa michango yao ya kujiunga na umoja na pia michango yao ya mwezi licha ya kwanza umoja na wana umoja wanajua kuwa nchi ina hali ngumu ila wengi wetu bado tuna kazi na vipato ambapo tunaweza fanya makubaliano na kamati ya fedha jinsi ya kumaliza pengo ulilo nalo katika michango yako.Kwa wale ambao bado hamjamaliza simu ya mwenyekiti wa fedha na mwenyekiti wa jumuiya iko mbioni kuikaribia simu yako ili ukumbushwe kufanya hivyo.Mwanachama hai lazima awe analipa michango yake ya jumuiya kama wengine.

Angenda ya pili:
Ilikuwa kuongelea suala la party ya usiku wa Mwafrika....ambapo mwenyekiti wa kamati ya Starehe hakuwepo kwenye kikao kutupa updates za kuhusu agenda hii,ingawa binafsi niliwahi wasiliana nae na mwenyekiti kwa kweli alikuwa busy sana na shule na aliomba kwa sasa hatoweza kutokana na ratiba yake ilivyo.Katibu wake bwana Edgar nae hakuwa na taarifa pia zaidi ya suala hili agenda hii ilirudishwa kwa wajumbe wa jumuiya na ilijadiliwa kama ifuatavyo mantiki mazima ya party hii.
Ilikuwa ni kuutangaza umoja hapa Canton na nje ya Canton kwa nyanja mbali mbali kiutamaduni,kiumoja, na kujenga jina la umoja ndani na nje ya Canton.Wana umoja walipendekeza Bw.Joe na Edgar na Martin waendeleze suala hili mpaka hapo mwenyekiti wa kamati hii atakapokuwa free tena kukamilisha suala hili.Ilikubalika kuwa mwezi Aprill ambapo ndio ilikuwa lengo haswa haitoweza fanyika mwezi huo kutokana na ukaribu wake kwahiyo uwezekano wa kuisogeza mbele ni mkubwa taarifa kamili watatupa hawa mabwana Joe na Edgar.

Agenda ya tatu:
Tulizungumzia suala la umoja kuandaa fomu maalumu za kujiunga na umoja na ( Joe alikuwa anazifanyia kazi) ili umoja uwe na records za kila mwanachama wake na zihifadhiwe kwenye safe box bank au safe bank lilinuliwe na kuwekwa mahali maalumu.Fomu hizi ni kwaajili ya basic infomations ambazo zitaonyesha anwani,majina kamili umeoa au hujaoa,mahali pa kazi na pia hiki kifungu kitakuwa kama option unaweza jaza ama usijaze info kama likitokea janga la msiba wapi mwili uhifadhiwe.Ingawa hili lilikuwa very sensitive kwa wajumbe ila njia hii ilionekana kila mtu ataipitia ni matter of time tu wajumbe waliombwa waende nalo tutakuwa tunayadiscuss kidogo kidogo katika vikao vyetu.

Agenda ya nne:
Joe alifafanua kwa kirefu na kwa utaalamu sana suala la life insurance na akasuggest kila mwanachama ni vyema awe nayo na tunaendelea na uchunguzi ili tupate moja ambayo itakuwa ya group kila mwanachama awe nayo na pia aliongelea suala la health insurance hili lilionekana ni lazima kila mwanachama awe na kazi ili kuwa nayo hii hamna alternative nyingine yeyote ile maana ni ghali sana.

Agenda ya Tano:
Katibu aliongelea kuhusu watu kuweka bayana mambo yao yanayohusu kupata misaada ya kiushauri kama ya uhamiaji,ndoa,wanasheria,tax nk.Kama wana umoja tunafanya kazi pamoja na lengo la umoja mwaka huu ni kila mwanachama anayefile na uhamiaji au aliyewahi file na hajafanikiwa afanikiwe kwa nguvu ya ushauri wa umoja.Umoja una nyezo nyingi ndani yetu pamoja na uchache wetu ila wanachama tulionao wana nyenzo za kutosha sana kuwasaidia wengine.Natoa mfano mtu kama Juma Msangi na Mohamed Sultan wanaufahamu wa kutosha sana kuhusu mambo ya talaka na dissolution ambayo hutahitaji mwanasheria na kulipa gharama kubwa sana lets avoid and use them.Joe ni nyenzo kubwa sana ndani ya Umoja kwa mambo mengi sana amekuwa msaada kwa wengi mwaka huu kuhusu suala zima la Tax returns,Martin Yohana ushauri wake ni asasi ya kutosha ndani ya chama na haswa suala zima la uhimizaji wa wtu kurudi shule,Frank uhamiaji ana idea za kutosha na wadada wengi na wakaka wengi ni wapishi wazuri sana.Edgar ni mtu mzuri sana katika kusimamia mambo muhimu na kuhakikisha yanaenda vizuri.Abeid amejitolea kwa wengi sana na pia umoja umekuwa unatumia nyumba yake kwa vikao.Zitto mcheshi mzuri ndani ya umoja.Gilly ni DJ wetu wa kutegemewa wa umoja na wengineo wengi.
Umoja una furaha kutangaza mwaka huu dada Edna na Suleiman wamepata green card mkiwaona wapeni hongera sana.

Pia tulipata wageni toka Columbus dada Oliva Kavishe na kaka Isaac Lyatuu walikuja na ujumbe ambao uliwapeleka viongozi Mansfield back in January.
Ujumbe wao ulikuwa kutambua kazi za watanzania ndani ya USA ambao wamefanya mengi kuliko kawaida kuwasaidia watanzania wengine wafanikiwe na jamii iwatambue.Balozi wa TANZANIA nchini Marekani anatarajiwa kuja katika sherehe hizo mwezi wa nne 26,2009.Itatumwa form kama survery watanzania watajaza majina ya watanzania wenzao ambao wanadhani wamefanya mengi kupita uwezo wao then itachujwa ili wapatikane waliochaguliwa na kupewa vyeti kwa kazi zao.

Asanteni,
Katibu.

No comments: